Chipukiz Cup, ni mashindano makubwa ya michezo yanayokutanisha vijana wenye vipaji kutoka ukanda wa nchi za Afrika Mashariki. Mashindano ya Chipukizi yamekua yakifanyika karibu kila mwaka, Mashindano hayo yamekua yakitoa nafasi kwa vijana wenye vipaji vya mpira wa miguu kuonesha uwezo wao. Mwaka huu (2024) mashindano yalifanyika nchini Tanzania, jijini Arusha, mnamo Desemba 9 hadi Desemba 15. Yakijumuisha timu za mpira wa miguu kwa vijana wa kike na wakiume. Mashindano haya pia yalijuimuisha mchezo wa kuogelea (Swimming) na mpira wa kikapu (Basketball). Kitu cha kipekee kuhusu mashindano haya kwa mwaka huu ni ushiriki wa kituo cha vijana cha Xavier, kikiwakilishwa na timu za mpira wa miguu: Timu ya wasichana chini ya umri wa Miaka 15 (U -15 girls) na timu ya wavulana chin ya umri wa Miaka 15 (U- 15 boys).
Mashindano ya Mwaka huu yalivuta hisia za kipekee ndani na nnje ya uwanja, yalifanyika katika mazingira yenye shangwe, furaha na hamasa. Timu shiriki zikonesha uthubutu an ari ya ushindani. Kwa kujivunia uwakilishi bora wa jamii zao, timu za wavulana na wasichana wa chini ya miaka 15 kutoka Kituo cha Vijana cha Xavier zilionesha azma na vipaji vya kuvutia licha ya ushindani mkali, timu zote mbili zilionesha mshikamano wa hali ya juu na uvumilivu, zikivutia hisia za timu nyingine.
Timu ya wasichana wa chini ya miaka 15 ilionesha umahiri wa kipekee ikishinda michezo yake yote ikisonga mbele na kuvuka hatua za Makundi. Hata hivyo safari yao ilifikia kilele katika hatua ya nusu fainali.
Wakati huohuo, timu ya wavulana wa chini ya miaka 15 pia ilionesha ushiriki bora, wakiubuka na ushindi katika mechi mbili, Sare moja na kupoteza mchezo mmoja, hii ikiwawezesha kuvuna alama 7 ambazo hazikutosha kuwavusha hatua ya robo fainali.
Mashindano ya Chipukizi Cup yamekua zaidi ya Mashindano kwa Vijana wa Xavier Youth Center. Mashindano haya yamekua ni jukwaa la urafiki,ushairi wa kimichezo, ukuaji wa kibinafsi na kumbukumbu zitakazoishi kwa kila mshiriki wa mashindano. Mashindano haya yanaweza kua ngazi wa vijana katika hatua muhimu za kuelekea fursa muhimu na kubwa zaidi katika maisha yao kwa kutumia vipaji vyao.